Monday, April 21, 2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Simu:022-2110146/2110150/2/211679 Faksi:022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
UTANGULIZI

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.

Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na 
Hisabati wa takribani walimu 26,000 kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/15 wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi/Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za serikali.

VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.

1:      MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:  MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA UFUNDI:  MUDA MIAKA 2.

(i)         Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na Monduli

Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa ‘Principal Pass’ mbili  katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.

(ii)        Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Kleruu
Mwombaji awe amehitimu:
a.   Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au
b.   Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

(iii)       Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na  ufaulu ‘Principal Pass’ mbili katika somo la ‘Agricultural science’ na ‘Biology’, ‘Chemistry’ au ‘Food and Nutrition’.


2:         MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA  MIAKA 3

Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa

Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.

3:         MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MUDA MIAKA 2.
(i)         Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.

Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha  ‘Principal Pass’ mbili


(ii)        Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja

(iii)       Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba.
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja

Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, Basic Applied Mathematics’, ‘General Studies’ na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.

4:      MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI: MUDA MIAKA 3)

Ualimu wa Stashahada ya  Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu

Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la I Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya ‘Mathematics’, ‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’,  ‘Agriculture’, ‘Food and Nutrition’, ‘English’ na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.


5.      MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2

Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na Monduli

Mwombaji awe amehitimu:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.


6:      MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI):- MUDA MIAKA 2.

(i)         Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.

Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika masomo ya ‘Biology, ‘Chemistry’ na ‘Food and Nutrition

(ii)        Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu

Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

(iii)       Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi
Mwombaji awe:

Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au

Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).


7:      MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA MSINGI:  MUDA MIAKA 2:

Ualimu wa Stashahada ya  Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

MAELEZO MUHIMU
(i)            Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)          Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
(iii)         Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(iv)         Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
(v)           Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vi)         Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu;

Namna ya kutuma maombi:
a)    Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO(online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz  AU  www.nacte.go.tz
Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tzna Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz

Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1.       Piga *150*00#
2.      Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3.      Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4.      Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5.      Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6.      Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7.      Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8.      Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
b)    Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

0 comments :

Post a Comment