Monday, November 26, 2012

Kocha mpya wa Chelsea, Rafael Benitez amesisitiza kuwa atafanikiwa kuzima uhasama kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambao walimpokea huku wakiwa wamebeba mabango ya kumsifu kocha laiyefutwa kazi. Mashabiki hao walimzomea Benitez, wakati alipojitokeza katika eneo linalotumiwa na maafisa wa kiufundi, na mashabiki wengine walimtusi wakati wa mechi yao dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City hiyo jana ambapo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kutofungana bao lolote. '' wakati mashabiki wanapoimba kuniunga mkono au kunikashifu, mimi sijali chochote. Kile ninachokitaka ni kubadili maoni yao'' alisema Benitez. Aliongeza kusema kuwa atafanya hivyo kwa kujitahidi zaidi na kuhakikisha kuwa Chelsea imeshinda mechi zake.
Habari zilizonifikia muda si mrefu zinasema msanii SHARO MILLIONEA AMEFARIKI DUNIA kutokana na ajali ya gari wakati akitoka mkoani Tanga. Tutawapa habari kutokana na jinsi tunavyoendelea kuzipata. namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe. rest in peace sharo
Mwezi huu, Majimbo mawili nchini marekani yamepiga kura kuhalalisha , kudhibiti na kutoza kodi bangi. Kutokana na matangazo ya kibiashara na sheria za kudhibiti ulevi wa bangi wakati madereva wakiwa njiani , basi tunahoji nini cha mno kinachosubiriwa? Kura iliyopigwa tarehe sita mwezi Novemba katika majimbo ya Colorado na Washington, bila shaka iliwatia furaha watumiaji wa Bangi lakini polisi wengi walilala wakiwa na wasiwasi si haba. Na hatua hiyo ikaleta karibu malumbano kati ya majimbo hayo mawili na serikali ya kitaifa, kwani bangi ingali imeharamishwa chini ya sheria za kitaifa. Lakini kama ilivyo ada, kila jimbo nchini Marekani liko huru kutunga sheria zake. Marijuana kama inavyojulikana na wengi, ni dawa ya kulevya inayotumiwa sana nchini Marekani. Lakini sasa wataalamu wanasema huu ni mwanzo tu wa kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ambayo bado imepigwa marufuku. “Hiki ni kionjo tu, bado mengi yatakuja’’ alisema Sanho Tree mkuregenzi mkuu wa mradi kuhusu sera ya mihadarati. "Ikiwa majimbo haya mawili yataendelea na harakati zao za kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya, bila mawingu kuanguka, basi utakuwa mwanzo mpya kwa uhuru wa kisiasa." Alisema Sanho

Thursday, November 8, 2012

......its the matter of time before the world get 2 know one among the greatest hiphop mc in sokoine university of agriculture....the bway is hot u know....he started his underground movements the couple of years back! and in this coming friday, he gona make the ground go down along side with some hiphop mc's like izo biznes n joh make....its d tym 2 make d campus go down!!! its time for kabalyrics to make d damn universe watch him....GOD WITH YOU BRO.
Kikosi kamili cha wachezaji hao 22 waliotangazwa na Poulsen akiwa jijini Mwanza leo ni: Makipa: Kaseja (Simba) na Deogratias Munishi (Azam) Mabeki: Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris na Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba). Viungo: Salum Abubakar “Sure Boy” (Azam), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji” na Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar). Washambuliaji: John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba) na Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe)
Stori za uhakika nilizozipata muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambae alikua anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana. Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012. Oktoba 23 2012 Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwaakisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
Wakati wimbo wa Diamond ‘nataka kulewa’ ukitengeneza topic kwenye media kibao TZ na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo wengi wanasema beat hiyo inafanana asilimia 100 na ile ya beat ya wimbo wa Pasha alomshirikisha Tunda Man ‘Mtoto Amekua’, Manecky wa AM records ambae ndiye aliyetengeneza ‘nataka kulewa’ amesema beat ya wimbo huo ni tofauti kabisa na ile ya wimbo wa Pasha. Producer huyo ambae ndiye mshindi wa kili music awards 2011 kama producer bora wa mwaka alifunguka kwa msisitizo kwenye XXL cha Clouds fm kuwa hakusample beat sehemu yeyote ile na hiyo beat aliifanya kwa mawazo yake mwenyewe kuanzia mwanzo kabisa. Alipoulizwa maoni yake kama beat hizo mbili zinafanana au hazifanani, alisema “kwa kitu ambacho mimi nimeweza kusikiliza hizi ni beat mbili tofauti, sema kuna idea ya lead sound ambayo inaweza kuwa na mfanano flani, ndio maana nikarudia kusema palepale, mimi ni mtu ambae nasikiliza muziki kila siku, na ni binadamu na sio computer sio kitu flani ambacho kinasema ni kitu flani kifanye hivi…!” Manecky amesema hata Tunda Man aliisikiliza ‘beat ya Nataka kulewa’ mara nyingi tu lakini hakuweza kuifananisha kabisa na ile ya wimbo wa Pasha ambao yeye mwenyewe kaweka vocal yake kwenye beat ileile inayofananishwa, lakini inaonekana alipousikia watu wanasema zinafanana ndipo na yeye akashtukia kuwa inawezekana iko hivyo.Duuuh..! Kweli tunatofautiana kushtukia copy, wengine wakisikia hata kinanda cha kwanza tu wanashtukia ila Tunda Man yeye ameshtuka baadae sana pamoja na kuitumia beat hiyo. Wimbo wa Diamond umepata challenge kubwa sana tangu au-release rasmi, muda mchache baada ya kuonekana beat inafanana na ya wimbo wa Pasha ft. Tunda Man ‘nataka kulewa’, H-Baba alijitokeza na kumtuhumu Diamond kwa kumuibia idea ya wimbo huo tena kwa makusudi huku akiweka hadharani vielelezo vya demo ya wimbo wake ‘nataka kulewa’ akiwa na Q-Chillah.
KITENDO cha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuwaambia walinzi wake kuwa kama hajatoa maagizo yoyote kwamba mama yake, Mariam Sepetu anakuja, akifika mlangoni asifunguliwe kimewashangaza wengi. Awali, Wema alieleza kuwa, ameweka utaratibu wa watu kuonana naye na kwamba wale watakaokwenda kwake bila taarifa watakuwa wanaishia getini. Maelezo hayo yalimfanya mwandishi wetu amuulize kama hata mama yake akienda kwake bila ‘apointimenti’ hawezi kuingia ndani ambapo alisisitiza kwa kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa watu wote akiwemo mzazi wake huyo. “Akija bila taarifa hawezi kuingia ndani. Si yeye tu, hata dada yangu, rafiki yangu yoyote yule, meneja wangu hata wewe kama sijatoa maagizo kwa walinzi basi ujue utaishia nje na ukinipigia simu huwa sipokei,” alisema Wema. Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya watu kumshangaa kwa kusema kuwa, utaratibu huo si mzuri kwani kufikia hatua ya kumtaka hadi mama yake aweke apointimenti ndipo amtembelee ni kutafuta laana.
hatimaye clement lugendo atoa blog yake........ni kijana mtanashati! mple na mcha Mungu... MUNGU IBARIKI TZ, MUNU IBARIKI SUA