Monday, November 26, 2012

Habari zilizonifikia muda si mrefu zinasema msanii SHARO MILLIONEA AMEFARIKI DUNIA kutokana na ajali ya gari wakati akitoka mkoani Tanga. Tutawapa habari kutokana na jinsi tunavyoendelea kuzipata. namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe. rest in peace sharo

0 comments :

Post a Comment