Friday, January 24, 2014

Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Indonesia kwa mwaka 2014/2015. Skolashipu hizo ni kwa kipindi cha kati ya miezi sita na/au mwaka mmoja. Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na wajaze fomu za maombi zinazopatikana kwenye Mtandao wa Serikali ya INDONESIA ufuatao http://www.eduicon.com/Scholarship/Details/82.html Fomu za maombi zilizokamilika kujazwa pamoja na viambatisho vilivyoainishwa ziwasilishwe kwenye Ubalozi wa Indonesia hapa Tanzania kabla ya tarehe 24/01/2014. 

SOURCE : Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM

0 comments :

Post a Comment