Watu watatu wamekufa baada ya gari walilokua wanalitumia kusombwa na maji
wakitokea katika kijiji cha Chilonwa Wilaya ya Chamwino Mkoani
Dodoma. Habari zilizotufikia kutoka dodoma kwa msemaji wa wilaya ya chamwino Richard Masimba aliwataja waliofariki ni Jane Ntimba , mkazi wa erea c, Sharifa Saidi ,na Sapiencia Augustino.
Gari hilo lenye usajili wa namba T694 BMA aina ya toyota asbuhi ya leo Hombolo.mmoja wao aliefanikiwa kuruko ni David Lukoka.
Tukio hilo pia
lilithibitishwa kutokea na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Ally,
wakati akizungumza na gazeti la majira akiwa eneo la tukio kwa njia ya simu.
“Sasa
hivi tuko eneo la tukio tukiwa na vifaa vya uokoaji lakini bado
tumeshindwa kulifikia hilo gari kwani limetitia kabisa, wakiangalia kwa
vifaa wanaligusa, lakini bado wameshindwa kulitoa,” alisema DC huyo.
“Kwa
kweli tunaomba Mungu atende miujiza yake kwani gari hilo limetumbukia
kwenye maji hayo tangu saa saba mchana na muda huu (saa 11. 30 jioni)
bado hawajatolewa.”
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, may your soul rest in peace SHARIFA SAID. Mbele yako, nyuma yetu. AMINA
0 comments :
Post a Comment