Monday, January 20, 2014

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinathibitisha kwamba Imetokea ajali mbaya huko Singida ambapo gari aina ya NOAH na Lori la mizigo yamegongana uso kwa uso na kisha gari hiyo aina ya NOAH kuingia chini ya uvungu wa Lori na kusababisha vifo vya watu hao 13 ambao wote walifia katika eneo la ajali.
 Taarifa inasema gari aina ya NOAH ilikuwa imebeba abiria kutoka Itigi wakielekea Singida Mjini.Inasemekana Dereva na utingo wa Lori walinusurika na walikimbia kusiko julikana mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.
SOURCE: ITV breaking News.

0 comments :

Post a Comment