Stori za uhakika nilizozipata muda mfupi uliopita ni kwamba mkali wa Hiphop kutoka A Town ambae alikua anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz, Isack Waziri (Lord Eyes) hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
Ametoka nje kwa dhamana toka ijumaa ya novemba 2 2012.
Oktoba 23 2012 Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alikaririwaakisema “Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
Thursday, November 8, 2012
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment