Monday, November 26, 2012

Kocha mpya wa Chelsea, Rafael Benitez amesisitiza kuwa atafanikiwa kuzima uhasama kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambao walimpokea huku wakiwa wamebeba mabango ya kumsifu kocha laiyefutwa kazi. Mashabiki hao walimzomea Benitez, wakati alipojitokeza katika eneo linalotumiwa na maafisa wa kiufundi, na mashabiki wengine walimtusi wakati wa mechi yao dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City hiyo jana ambapo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kutofungana bao lolote. '' wakati mashabiki wanapoimba kuniunga mkono au kunikashifu, mimi sijali chochote. Kile ninachokitaka ni kubadili maoni yao'' alisema Benitez. Aliongeza kusema kuwa atafanya hivyo kwa kujitahidi zaidi na kuhakikisha kuwa Chelsea imeshinda mechi zake.

0 comments :

Post a Comment