Mwezi huu, Majimbo mawili nchini marekani yamepiga kura kuhalalisha , kudhibiti na kutoza kodi bangi.
Kutokana na matangazo ya kibiashara na sheria za kudhibiti ulevi wa bangi wakati madereva wakiwa njiani , basi tunahoji nini cha mno kinachosubiriwa?
Kura iliyopigwa tarehe sita mwezi Novemba katika majimbo ya Colorado na Washington, bila shaka iliwatia furaha watumiaji wa Bangi lakini polisi wengi walilala wakiwa na wasiwasi si haba.
Na hatua hiyo ikaleta karibu malumbano kati ya majimbo hayo mawili na serikali ya kitaifa, kwani bangi ingali imeharamishwa chini ya sheria za kitaifa. Lakini kama ilivyo ada, kila jimbo nchini Marekani liko huru kutunga sheria zake.
Marijuana kama inavyojulikana na wengi, ni dawa ya kulevya inayotumiwa sana nchini Marekani. Lakini sasa wataalamu wanasema huu ni mwanzo tu wa kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ambayo bado imepigwa marufuku.
“Hiki ni kionjo tu, bado mengi yatakuja’’ alisema Sanho Tree mkuregenzi mkuu wa mradi kuhusu sera ya mihadarati.
"Ikiwa majimbo haya mawili yataendelea na harakati zao za kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya, bila mawingu kuanguka, basi utakuwa mwanzo mpya kwa uhuru wa kisiasa." Alisema Sanho
Monday, November 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment